Nape Nnauye aeleza alichoambiwa na Tundu Lissu wakitoka bungeni jana
Mbunge
wa Mtama (CCM), Nape Nnauye ameeleza alichoambiwa na Mbunge wa Singida
Mashariki (Chadema), Tundu Lissu jana Alhamisi mchana wakati wakitoka
bungeni huku wakicheka.
Nape amesema Lissu alimwambia, “Wewe
Nape ni mjomba wangu, kwa nini unabaki CCM? Mimi na wewe tunafuatiliwa
na jamaa zako wakitumia gari moja. Mimi na wewe ni watuhumiwa, hama CCM
mjomba.”
Lissu
alipigwa risasi jana Alhamisi mchana na kupelekwa chumba cha upasuaji
katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na baadaye usiku alihamishiwa
Hospitali ya Aga Khan ya Nairobi nchini Kenya.
Mbunge
wa Rombo, Joseph Selasini jana wakati Lissu akipelekwa Kenya alisema
ameambatana na mkewe, madaktari wawili wasio na mipaka; Mwenyekiti wa
Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter
Msigwa.
Ndege iliyomsafirisha iliondoka katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma saa sita na robo usiku.
Nape Nnauye aeleza alichoambiwa na Tundu Lissu wakitoka bungeni jana
Reviewed by RICH VOICE
on
Septemba 08, 2017
Rating:
Hakuna maoni