Waziri Mkuu Kesho kuzindua mfumo wa uandaaji bajeti
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa Jumanne Septemba 5 atazindua mifumo miwili
itakayosaidia kuongeza ufanisi na kupunguza gharama wakati wa
ufuatiliaji na uandaaji wa bajeti nchini.
Katika
uzinduzi huo, mawaziri sita ambao wanafanya kazi na Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) watahudhuria.
Kiongozi
wa timu ya rasilimali fedha, Dk Gemini Mtei amesema uzinduzi huo
utahudhuriwa na Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene; Waziri wa Fedha
na Mipango, Dk Philip Mpango; Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (sera, bunge, kazi, vijana, na watu wenye ulemavu), Jenista
Mhagama.
Ofisa
Usimamizi Mwandamizi wa Fedha Tamisemi, Elisa Rwamingo amesema mfumo
huo utatumika katika halmashauri zote 185. Amesema wakuu wa vitengo
katika halmashauri wamepatiwa mafunzo ya utumiaji wa mfumo huo, ambao
wataenda kuwafundisha watumishi wengine.
Waziri Mkuu Kesho kuzindua mfumo wa uandaaji bajeti
Reviewed by RICH VOICE
on
Septemba 04, 2017
Rating:
Hakuna maoni