Waziri Makamba amlilia Muhingo Rweyemamu
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January
Makamba amemtaja mwandishi wa habari mkongwe, Muhingo Rweyemamu kuwa
alikuwa mwalimu na mshauri wake wa karibu.
Mara
baada ya kumaliza kusaini kitabu cha wageni waliohudhuria msiba wa
mwandishi huyo nyumbani kwake Mbezi Luis, January alisema alifanya kazi
na Muhingo kwa karibu wakati wa uongozi wa awamu ya nne chini ya Rais
Jakaya Kikwete.
Muhingo amewahi kuwa mkuu wa wilaya tatu kwa vipindi tofauti; Handeni, Makete na Morogoro.
“Namkumbuka
kwa mambo mengi alikuwa ni mtu anayepen-da kuelimisha, alikuwa
akinishauri hata kusoma vitabu vya kunisaidia kunipa mwongozo,”
alisema.
Alisisitiza kuwa anaamini wana tasnia ya habari watamuenzi
kwa kuendelea kuandika habari zenye weledi kwa manufaa ya jamii na Taifa kwa ujumla.
Kaka wa marehemu, Elisa Muhingo alisema kifo cha mdogo
wake ni pigo kubwa kwa familia kwa sababu alikuwa tegemeo lao.
“Lakini
kwa jinsi alivyougua, ameteseka kwa maumivu makali, kifo chake
tusingeweza kukipinga. Tunamshukuru Mun-gu amempumzisha, tunatafakari na
kujipanga kuishi bila yeye,” alisema.
Aliyekuwa
rafiki wa karibu wa marehemu ambaye pia ni mwandishi mkongwe, Absalom
Kibanda alisema leo wanatarajia kuuhamisha mwili kutoka chumba cha maiti
cha Hospitali ya Aga Khan alikofia na kuupeleka nyumbani kwake kwa
maandal-izi ya maziko.
“Baada
ya kikao cha mashauriano, imekubaliwa kwamba Rweyemamu atazikwa katika
makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam siku ya Jumanne, Septemba 5,
2017,” alisema.
Alisema
shughuli za mazishi zitatanguliwa na ibada ya kumuaga ambayo itafanyika
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tan-zania (KKKT) Mbezi, Kibanda cha
Mkaa.
Waziri Makamba amlilia Muhingo Rweyemamu
Reviewed by RICH VOICE
on
Septemba 03, 2017
Rating:
Hakuna maoni