Rugemalira wa Escrow agonga mwamba Mahakama ya Mafisadi
Mshtakiwa
wa kesi ya uchotaji fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow, James
Rugemalira amegonga ukuta katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya
Rushwa na Uhujumu Uchumi (Mahakama ya Mafisadi) baada ya kunyimwa
dhamana.
Rugemalira
ambaye anakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
yenye mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana, alikimbilia
mahakamani hapo kuomba afutiwe mashtaka ya utakatishaji fedha kisha
aachiwe huru kwa dhamana kwa madai hati ya mashtaka yanayowakabili ina
kasoro za kisheria.
Jana,
Jaji Mfawidhi Firmin Matogolo alitupilia mbali maombi hayo akisema
Mahakama hiyo haina mamlaka ya kumpa nafuu alizokuwa akiziomba.
Wakati
wa usikilizwaji wa maombi hayo, jopo la mawakili wa Rugemalira
waliieleza Mahakama kuwa hati ya mashtaka haina maelezo yanayoonyesha
kosa la utakatishaji fedha.
Hata
hivyo, Wakili wa Serikali Mkuu, Dk Zainabu Mango alipinga hoja hizo,
akidai mashtaka yanayomkabili mshtakiwa hayana dhamana.
Akijibu hoja ya kasoro za hati ya mashtaka, Wakili Mango alidai maombi hayo yamepelekwa kwenye jukwaa ambalo si sahihi.
Alisema
kesi hiyo haijafikia hatua ya kusikilizwa katika mahakamani hiyo na
kwamba inaweza kuangalia uhalali wa mashtaka hayo, shauri hilo
litakapohamishiwa mahakamani hapo kwa usikilizwaji.
Hata
hivyo, Jaji alikubaliana na hoja za Wakili Mango kuwa Mahakama hiyo
haina mamlaka ya kuchunguza uhalali wa hati ya mashtaka kwa kuwa suala
hilo limefikishwa wakati ambao si muafaka.
Pia,
Jaji Matogolo alisema kwamba Mahakama hiyo huwa na mamlaka ya
kuchunguza uhalali wa mashtaka endapo maombi yangewasilishwa kwa njia ya
mapitio na si dhamana.
Rugemalira
na mshirika wake wa Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power
Tanzania Limited (IPTL), Harbinder Singh Sethi wanakabiliwa na kesi ya
uhujumu uchumi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Rugemalira wa Escrow agonga mwamba Mahakama ya Mafisadi
Reviewed by RICH VOICE
on
Septemba 01, 2017
Rating:
Hakuna maoni