Waandamanaji wakesha kupinga utawala wa Gnassingbe Togo
Vikosi vya usalama nchini Togo
vimerusha gesi ya kutoa machozi mapema leo, kutawanya mamia ya
waandamaji wanaoipinga seikali walioshinda usiku kucha mjini Lome.
Vyombo vya habari vimekuwa vikichapisha picha za waandamanaji wakilala barabarani usiku.Polisi walichukua hatua ya maandamano ya nchi nzima ya saa 48 ya kutaka kumalizika kwa utawala wa miaka 50 wa familia ya Gnassingbe
Hakuna taaraifa yoyote ya majeruhi au maafa.
Maandamano yaliendelea licha ya Rais Faure Gnassingbe, kuahidi kurejesha sheria ya kutaka rais ahudumu kwa mihula miwili pekee nchini humo.
Mamlaka zimeamrisha kuzimwa kwa mitandao kwa muda wa siku mbili kama njia ya kukabiliana na maandamano hayo.
Waandamanaji wakesha kupinga utawala wa Gnassingbe Togo
Reviewed by RICH VOICE
on
Septemba 08, 2017
Rating:
Hakuna maoni