Update Toka kwa Mbowe: Tundu Lissu Kwa Sasa Anaweza Kuongea na Kula Kidogo
Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa hivi sasa Mbunge wa Singida
Mashariki, Tundu Lissu anaweza kuongea na kula kidogo.
Akizungumza
na waandishi leo Alhamisi jijini Nairobi, Mbowe amesema taarifa za
kwamba Lissu amepata maambukizi katika kifua ambayo yanatishia maisha
yake siyo za ukweli.
Mbowe amesema hali ya Lissu inabadilika kila siku hivyo amewahakikishia wananchi kuwa anaendelea kurejea katika hali yake.
Amesema Lissu ameweza kuonana na baadhi ya waliomtembelea kwa maelekezo ya madaktari ambao wanamtibu.
"Pamoja
na kwamba kuna watu wengi wanataka kumuona lakini ni wachache
wanaoruhusiwa kumuona kwa kuwa madaktari wanataka apumzike,"amesema
Mbowe.
Update Toka kwa Mbowe: Tundu Lissu Kwa Sasa Anaweza Kuongea na Kula Kidogo
Reviewed by RICH VOICE
on
Septemba 14, 2017
Rating:
Hakuna maoni