Harbinder Sethi wa Escrow kawekewa Maputo tumboni
Wakili
wa mshtakiwa Harbinder Sethi, Joseph Makandege ameulalamikia upande wa
Jamhuri kwa kushindwa kumpeleka mteja wake Hospitali ya Taifa Muhimbili
kama Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ilivyoamuru.
Amedai
hali hiyo inahatarisha afya ya mteja wake kwani akikosa kupata matibabu
sahihi anaweza kupoteza maisha kutokana upasuaji aliofanyiwa
uliosababisha kuwekewa maputo tumboni.
“Mara
mbili mahakama ilitoa amri ikielekeza utawala wa Magereza kumpeleka
mshtakiwa wa kwanza Muhimbili , amri ilitolewa baada ya mahakama
kukubaliana na hoja za upande wa utetezi, lakini badala ya kumpeleka
Muhimbili, Magereza walimpeleka mshtakiwa Hospitali ya Amana.
“Kwa
taarifa za kitabibu ni kwamba hali ya mshtakiwa wa kwanza isipohudumiwa
ipaswavyo inaweza kusababisha kifo kwani maputo yanaweza kupasuka
tumboni , mahakama iliekeza mshtakiwa apelekwe moja kwa moja Muhimbili
ambayo ni hospitali ya juu kabisa ya Serikali, ndio nategemea inaweza
kuwa na wataalamu na vifaa thabiti kwa ajili ya matatizo yanayomkabili
mshtakiwa wa kwanza,” amedai.
Makandege
alidai amri zote zilizotolewa na mahakama hazijatekelezwa , aliomba
mahakama itoe amri nyingine ya kuutaka upande wa Jamhuri kuamuru amri
iliyotolewa itekelezwe.
Akijibu
Wakili wa Serikali Mkuu, Vitalis Peter amedai Jamhuri haijakaidi amri
ya mahakama na kwamba Magereza wana utaratibu wao ambapo wanahojiana na
mgonjwa wakiona tatizo lake hawana utaalamu nalo wanampa rufaa kwenda
Muhimbili. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 14 mwaka huu kwa ajili
ya kutajwa.
Washtakiwa
katika kesi hiyo mshtakiwa Seth na James Rugemarila, wanakabiliwa na
kesi ya uhujumu uchumi ikiwa na mashitaka 12 yakiwemo ya kutakatisha
fedha hivyo kuwafanya wakose dhamana.
Harbinder Sethi wa Escrow kawekewa Maputo tumboni
Reviewed by RICH VOICE
on
Septemba 01, 2017
Rating:
Hakuna maoni