Breaking News: Mahakama Yamuachia Huru Yusuf Manji
Mahakama
imemuachia huru mfanyabiashara Yusuf Manji katika kesi ya uhujumu
uchumi baada ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) kuwasilisha hati
mahakamani hapo ikionyesha kuwa hana nia ya kuendelea na kesi dhidi
yake.
Manji
na watuhumiwa wenzake watatu walikuwa wakikabiliwa na mashtaka saba
yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa
Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ)
na wa Commanding Officer Korogwe na plate number mbili za magari ya
serikali.
Watuhumiwa
wengine walioachiwa huru kwenye kesi hiyo ni Deogratius Kasinda na
Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja.
Breaking News: Mahakama Yamuachia Huru Yusuf Manji
Reviewed by RICH VOICE
on
Septemba 14, 2017
Rating:
Hakuna maoni