Rais Museveni aagiza uchunguzi Ufanyike Kubaini chanzo cha ajali iliyoua Watanzania 13
Rais
Yoweri Museveni wa Uganda amesema upelelezi kubaini sababu za ajali
iliyosababisha vifo vya Watanzania 13 waliokuwa wakitoka harusini nchini
humo unaendelea.
Waziri
wa Ofisi ya Rais anayeshughulikia Jiji la Kampala, Bety Kamya akisoma
salamu za rambirambi kutoka kwa Rais Museveni amesema licha ya kutoa
pole kwa familia, kiongozi huyo ameagiza uchunguzi wa sababu za ajali
ufanyike.
Amesema pia amewapongeza maharusi, Dk Aneth na Dk Trease Ibingira na amewatakiwa maisha mema ya ndoa.
Mbali ya hilo, amesema anawaombea ili kukabiliana na kipindi kigumu walichonacho.
Amesema Rais anawashukuru Watanzania kwa kuwa wavumilivu katika kipindi kigumu cha kupoteza wapendwa wao.
"Nakabidhi
vyeti hivi vya vifo vya ndugu zetu 13 nawapa pole sana," amesema Waziri
Kamya akimkabidhi vyeti hivyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na
Utawala Bora, Angellah Kairuki.
Waziri
Kairuki amesema Rais John Magufuli amepokea taarifa ya vifo hivyo kwa
mshtuko na alitoa maelekezo ya kupokewa miili hiyo, kuhifadhiwa kwenye
Hospitali ya Jeshi Lugalo, kuagiwa hapo na kusafirishwa kwa maziko.
Amesema maagizo hayo wanaendelea kuyatekeleza ikiwa ni pamoja na kutoa magari kwa ajili ya kusafirisha miili hiyo.
Waziri Kairuki amesema kwa namna isiyo katika wakati wa kawaida, anawapongeza maharusi na kuwatakia maisha mema.
"Haya ni mapenzi ya Mungu, hili lisiwanyong'onyeshe maharusi," amesema Kairuki.
Ameishukuru Serikali ya Uganda kwa kukodi ndege kuirudisha nyumbani miili hiyo.
Rais Museveni aagiza uchunguzi Ufanyike Kubaini chanzo cha ajali iliyoua Watanzania 13
Reviewed by RICH VOICE
on
Septemba 20, 2017
Rating:
Hakuna maoni