Kimbunga Irma chaendelea na uharibifu mkubwa huko Caribbean

Kimbunga Irma kimeelekea visiwa vya
Turks na Caicos baada ya kusababisha uharibifu mkubwa huko Caribbean na
kuwaua takriban watu 14.
Visiwa
vilivyo nyanda za chini vinaripotiwa kuwa kwenye hatari kubwa kukiwa na
uwezekano wa kupigwa na mawimbi ya hadi urefu wa mita 6 kuliko viwango
vya kawaida.Kumeripotiwa uharibifu na mafuriko nchini Haiti ambapo miundo mbinu bado ni mibaya tangu litokee tetemeo la ardhi mwaka 2010.
Irma ni kimbunga cha kiwango cha tano.
Hiki ndicho kiwango cha juu zaidi cha kimbunga na upepo wake una kasi ya kilomita 280 kwa saa.
Kuna wasi wasi kuwa ugonjwa unaweza kusambaa kwa haraka maeneo ambapo maji ya kunywa na huduma za usafi zimeathirika, na maafisa wameonya kuwa idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka.
Nchini Cuba maelfu ya watalii kutoka maeneo ya kistarehe ya pwani wamehamishwa.
Kimbunga Irma chaendelea na uharibifu mkubwa huko Caribbean
Reviewed by RICH VOICE
on
Septemba 08, 2017
Rating:
Hakuna maoni