BREAKING NEWSSSSSSSSS :Mlipuko Kagera Tanzania waua wanafunzi sita

Watu zaidi ya 25 wamejeruhiwa baada ya mlipuko
Image captionWatu zaidi ya 25 wamejeruhiwa baada ya mlipuko
Wanafunzi sita wa shule ya msingi Kihinga mkoani Kagera kaskazini magharibi mwa Tanzania wamefariki dunia na wengine zaidi ya 40 wamejeruhiwa baada ya kulipukiwa na bomu wakicheza.
Kamanda wa polisi wa mkoa, Augustine Orom huo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari wananchi wamejitokeza kuchangia damu kwa ajili ya kuwasaidia majeruhi.
Kwa mujibu wa Dokta Mariagoreth Fredrick ambaye ni mganga mkuu hosipitali ya Rurenge, amethibitisha kupokea miili hiyo na majeruhi ambao baadhi wako katika hali mbaya na tayari wanapatiwa matibabu.
"Tulionao hali ya sio nzuri. Wengine wameumia matumbo, wengine wamechanika bandama, wengine wamevunjika miguu, wengine vichwa vimepata majeraha, wengine wameumia macho." Dokta Mariagoreth ameiambia BBC.
Inaelezwa kwamba kabla ya kulipukiwa na kifaa hicho kinachoarifiwa kuwa ni bomu, wanafunzi hao walikuwa wanakichezea.
Taarifa zaidi zinafuata.CHANZO BBC SWAHLI
BREAKING NEWSSSSSSSSS :Mlipuko Kagera Tanzania waua wanafunzi sita BREAKING NEWSSSSSSSSS :Mlipuko Kagera Tanzania waua wanafunzi sita Reviewed by RICH VOICE on Novemba 08, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...