taarifa nyingine ni kwamba Mlipuko Kagera Tanzania waua wanafunzi sita

Baadhi ya wajeruhi wakipata matibabu katika hosipitali ya Rulenge, Ngara
Haki miliki ya pichaSHABANI NDYAMKAMA
Image captionBaadhi ya wajeruhi wakipata matibabu katika hosipitali ya Rulenge, Ngara
Wanafunzi sita wa shule ya msingi Kihinga mkoani Kagera kaskazini magharibi mwa Tanzania wamefariki dunia na wengine 41 wamejeruhiwa baada ya kulipukiwa na bomu wakicheza.
Kamanda wa polisi wa mkoa, Augustine Orom huo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari wananchi wamejitokeza kuchangia damu kwa ajili ya kuwasaidia majeruhi.
Watoto wakipata huduma katika hosipitali ya Rulenge baada ya mlipukoHaki miliki ya pichaSHABANI NDYAMKAMA
Image captionWatoto wakipata huduma katika hosipitali ya Rulenge baada ya mlipuko
Kwa mujibu wa Dokta Mariagoreth Fredrick ambaye ni mganga mkuu hosipitali ya Rulenge, amethibitisha kupokea miili hiyo na majeruhi ambao baadhi wako katika hali mbaya na tayari wanapatiwa matibabu.
"Tulionao hali ya sio nzuri. Wengine wameumia matumbo, wengine wamechanika bandama, wengine wamevunjika miguu, wengine vichwa vimepata majeraha, wengine wameumia macho." Dokta Mariagoreth ameiambia BBC.
Inaelezwa kwamba kabla ya kulipukiwa na kifaa hicho kinachoarifiwa kuwa ni bomu, wanafunzi hao walikuwa wanakichezea.
taarifa nyingine ni kwamba Mlipuko Kagera Tanzania waua wanafunzi sita taarifa nyingine ni kwamba Mlipuko Kagera Tanzania waua wanafunzi sita Reviewed by RICH VOICE on Novemba 08, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...