Papa Francis aanza ziara Myanmar

Papa Francis akiwa na kiongozi mkuu wa wa Myanmar Aung San Suu Kyi

Image captionPapa Francis akiwa na kiongozi mkuu wa wa Myanmar Aung San Suu Kyi
Papa Francis ameanza ziara yake nchini Myanmar, ambapo amekutana na mkuu wa jeshi katika siku ya kwanza ya ziara yake katika nchi inatuhumiwa kutokana na vitendo wanavyofanyiwa watu wa jamii ya Kiislam ya Rohingya.
Generali Aung Hlaing ametupilia mbali madai kuwa kuna ubaguzi wa kidini katika operesheni za kijeshi zinazoendelea katika jimbo la Rakhine.
Hata hivyo maofisa wengi kutoka jamii wa watu wa Budha nchini humo wanasubiria kuona kama Papa atazungumzia vipi mgogoro wa Rohingya.
Kumekuwa na msukumo mkubwa dhidi ya papa Francis kutoka serikali za mataifa mengine na makundi ya haki za binadamu kuhakikisha anaweka msukumo kuhusiana na suala la Rohingya.
Zaidi ya watu laki sita wamekimbia kutoka Myanmar na kwenda nchi jirani Burma na Bangaladesh tangu mwezi Agosti kutokana na mauajia yanayodaiwa kufanywa na jeshi.
Papa Francis aanza ziara Myanmar Papa Francis aanza ziara Myanmar Reviewed by RICH VOICE on Novemba 28, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...