TUNISIA YATOA SARE TASA NA LIBYA NA KUKATA TIKETI YA KOMBE LA DUNIA

Tunisia imekata tiketi ya kucheza fainali za kombe la dunia baada ya kutoka na pointi moja dhidi ya majirani zao Libya hapo jana katika mchezo ulioishia kwa sare ya 0-0.

Tunisia imemaliza ikiwa na pointi 14 katika kundi A, ikiwa mbele ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iliyoshinda magoli 3-1 dhidi ya Guinea Jijini Kinshasa.

Tunisia ambayo haikufungwa imeshashiriki mara nne katika fainali za kombe la dunia na ilikuwa timu ya kwanza Afrika kushinda mchezo katika michuano hiyo mwaka 1978.
TUNISIA YATOA SARE TASA NA LIBYA NA KUKATA TIKETI YA KOMBE LA DUNIA TUNISIA YATOA SARE TASA NA LIBYA NA KUKATA TIKETI YA KOMBE LA DUNIA Reviewed by RICH VOICE on Novemba 13, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...