Raia wajitokeza kumshinikiza Mugabe kujiuzulu Zimbabwe

Raia wajitokeza Zimbabwe kumshinikiza Mugabe kung'atuka mamlakani



Haki miliki ya pichaEPA
Image captionRaia wajitokeza Zimbabwe kumshinikiza Mugabe kung'atuka mamlakani

Maelfu ya raia wa Zimbabwe wamejitokeza barabarni hasa mjini Harare wakijiandaa kwa mkutano mkubwa unaoungwa mkono na chama tawala ZANU-PF katika jitihada za kuongeza shinikizo za kumtaka rais Mugabe ajiuzuulu,wakishikilia mabango yaliyoandikwa Mugabe Must Go.
Zanu-PF ndio chama kilichomsaidia Mugabe kuwa madarakani nchini kwa takriban miaka 40.
Lakini sasa inabidi wamshinikize ajiuzulu kufuatia mpasuko mkubwa katika chama tawala.
Kikubwa kinachozozaniwa ni nani atakayemrithi rais Mugabe atakapoochia madaraka.
Jeshi la nchi hiyo lilichukua hatamu za kiserikali na kumweka Mugabe chini ya kizuizi cha nyumbani tangu juzi na wamekuwa wakifanya mazungumzo ya kina.
MUgabe angependelea mkewe kumrithi lakini wapiganiaji wa uhuru nchini humo wanamtaka aliyekuwa makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa ambaye Mugabe alimfuta kazi wiki iliyopita, kutokana na uhasama mkubwa baina yake na mkewe rais Mugabe uliotokana na upiganiaji huo wa madaraka.
Zaidi ya hayo Bw. Mugabe angependa kuendelea kuwa uongozini hadi chama kitakapofanya mkutano wao mkuu mwezi ujao.
Raia wajitokeza kumshinikiza Mugabe kujiuzulu Zimbabwe Raia wajitokeza kumshinikiza Mugabe kujiuzulu Zimbabwe Reviewed by RICH VOICE on Novemba 18, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...