Magufuli aagiza kubomolewa kwa jengo la shirika la kuzalisha Umeme, Tanesco.

Makao makuu ya shirika la kuzalisha na kusambaza umeme, TANESCO

Haki miliki ya pichaTANESCO
Image captionMakao makuu ya shirika la kuzalisha na kusambaza umeme, TANESCO
Katika ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa barabara katika eneo la Ubungo mjini Dar es salaam,Rais Magufuli ameagiza sehemu ya jengo ambalo ni makao makuu ya shirika linalozalisha na kusambaza umeme, TANESCO, kuwekwa alama ya 'X' kuashiria jengo hilo libomelewe.
Jengo jingine ambalo litaathiriwa na agizo hilo ni jengo la wizara ya maji ambalo lipo jirani.
Imeagizwa majengo hayo kubomolewa kutokana na kuwa yamejengwa katika sehemu ya hifadhi ya barabara.
Zoezi la bomoa boma limekuwa likiendelea, ambapo majengo pembezoni ya barabara inayounganisha mji wa Dar es salaam na maeneo mengine ya nchi yameathirika. Wakaazi wengi waliokuwa wakiishi katika maeneo yanayodaiwa kuwa katika hifadhi ya barabara wamepoteza makazi yao.
Magufuli aagiza kubomolewa kwa jengo la shirika la kuzalisha Umeme, Tanesco. Magufuli aagiza kubomolewa kwa jengo la shirika la kuzalisha Umeme, Tanesco. Reviewed by RICH VOICE on Novemba 15, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...