Mwanajeshi wa Korea Kaskazini aliyepigwa risasi 6 akitoroka apata afueni

Mwanajeshi wa Korea Kaskazni akikimbizwa hospitali baada ya kupigwa risasi sita na wanajeshi wa taifa lake alipokuwa akitoroka

Haki miliki ya pichaEPA
Image captionMwanajeshi wa Korea Kaskazni akikimbizwa hospitali baada ya kupigwa risasi sita na wanajeshi wa taifa lake alipokuwa akitoroka
Mwanajeshi mmoja wa Korea Kaskazini ambaye alipigwa risasi 6 alipokuwa akivuka mpaka wa nchi hiyo, katika harakati za kutoroka, amepata afueni na sasa anaweza kuwasiliana na wahudumu wa kimatibabu.
Madaktari wanasema kuwa wamemtaka atizame runinga na kwa sasa anaonyeshwa filamu za Korea Kaskazini.
Wiki iliyopita, askari huyo aliamua kulitoroka taifa hilo, kwa ujasiri mkubwa, ili kuingia kwenye ardhi ya taifa jirani la Korea Kusini, hatua iliyowalazimu wanajeshi wenzake kummiminia zaidi ya risasi 40, huku sita zikimpata.
Wengi walidhani amefariki, lakini kwa kudra za mwenyezi Mungu, yungali hai.
Wafanyikazi katika Hospitali hiyo wanasema kuwa japo askari huyo anahuzuni nyingi, wamemwekea bendera ya Korea Kaskazini ukutani karibu na kitanda chake, ili kumliwaza.
Mwanajeshi wa Korea Kaskazini aliyepigwa risasi 6 akitoroka apata afueni Mwanajeshi wa Korea Kaskazini aliyepigwa risasi 6 akitoroka apata afueni Reviewed by RICH VOICE on Novemba 21, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...