Kenya yailalamikia Tanzania juu ya mifugo waliopigwa mnada

Waziri wa maswala ya nchi za kigeni Kenya Amina Mohammed

Image captionBi Amina Mohamed amesema mazungumzo bado yanaendelea
Waziri wa mambo ya nje nchini Kenya Amina Mohamed ameilalamikia serikali ya Tanzania kufuatia hatua ya taifa hilo kuwapiga mnada zaidi ya ng'ombe 1,300 walioingia nchini humo kinyume na sheria.
Serikali ya Rais John Magufuli ilichukua hatua hiyo baada ya wafugaji kuingia nchini humo na mifugo wao wakitafuta lishe.
Hatua hiyo inajiri siku moja tu baada ya Rais Magufuli kusema kuwa taifa hilo sio shamba la mifugo wa taifa jirani.
Akizungumza katika mkoa wa Kagera ambako alikuwa katika ziara yake ya kikazi Magufuli alisema kwamba Tanzania sio shamba la kuchungia mifugo ya nchi jirani na kwamba ataichukulia mifugo hiyo hatua kali za kisheria.
Vilevile alizitaka nchi Jirani kuchukua hatua kama hiyo iwapo mifugo ya Tanzania wataingia katika mataifa hayo kinyume na sheria.
Hatua ya kuwapiga mnada ng'ombe hao ilizua hisia kali miongoni mwa wafugaji wa Kenya baada ya wenzao waliokuwa na mifugo hao kukamatwa na kuzuiliwa kwa kuingia nchini humo kinyume na sheria.
Na kufuatia hatua hiyo waziri wa mambo ya nje nchini Kenya Amina Mohammed alidaiwa kuanzisha mazungumzo kati ya serikali hizi mbili kutatua mzozo huo, mazungumzo ambayo yalishindwa kufua dafu.
''Tulidhani kwamba mazungumzo ya kidiplomasia yangetatua mzozo huu, lakini tulishindwa kuafikia makubaliano. Ni wakati huo ambapo tuliamua kuzungumza na balozi wetu nchini humo kuwasilisha barua ya kupinga hatua ya kuwapiga mnada mifugo hao''.
''Historia ambayo tumekuwa nayo na Watanzania ni nzuri sana na kila kunapotokea tatizo tumekuwa tukitatua.Ni kwa sababu hiyo ambapo imekuwa hatua ya kushangaza miongoni mwa wafugaji wa Kenya'', waziri huyo alizungumza katika mkutano na vyombo vya habari.
Wafugaji wa Kenya wapata hasara kwa kuingiza ngombe zao Tanzania
Bi Mohamed amesema kuwa Kenya imekuwa ikiwavumilia wafugaji wa nchi jirani ambao wamekuwa wakivuka na kuingia katika eneo la Kajiado nchini Kenya kwa wingi.
''Barua yetu ya pingamizi ni kuonyesha wasiwasi wetu kuhusu kisa kilichotokea licha ya kuwepo katika mazungumzo, tunatumai tutasuluhisha tatizo hili'', alisema waziri Mohamed.
Mazungumzo baina ya nchi hizo mbili bado yanaendelea.
Kenya yailalamikia Tanzania juu ya mifugo waliopigwa mnada Kenya yailalamikia Tanzania juu ya mifugo waliopigwa mnada Reviewed by RICH VOICE on Novemba 08, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...