TIMU YA ARSENAL YACHARUKA YAMPIGA MTU MKONO


Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, amempongeza mpambanaji Mesut Ozil baada ya raia huyo wa Ujerumani kuchangia ushindi mnono wa klabu hiyo wa magoli 5-0 dhidi ya Huddersfield.



Ozil alifunga goli moja na kusaidia mengine mawili na kuifanya Arsenal kushinda michezo saba ya Ligi Kuu ya Ungereza katika msimu huu.




           Mshambuliaji Mfaransa Alexandre Lacazette akiifungia Arsenal goli la kwanza



Mohamed Salah ametokea benchi na kufunga mara mbili na kuisaidia Liverpool kupata ushindi wa ugenini wa magoli 3-0 dhidi ya Stoke City na kukwea hadi katika nafsi ya nne.



Winga raia wa Senegal Sadio Mane aliwapatia Liverpool goli la kwanza la utata akitumbukiza mpira wavuni sekunde chache kabla ya refa msaidizi kutoa uamuzi.



Katika mchezo huo Stoke waliamini kipa wa Liverpool, Simon Mignolet, alipaswa kutolewa nje kwa kumchezea rafu mshambuliaji Mame Biram Diouf nje ya boksi.
TIMU YA ARSENAL YACHARUKA YAMPIGA MTU MKONO TIMU YA ARSENAL YACHARUKA YAMPIGA MTU MKONO Reviewed by RICH VOICE on Novemba 30, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...