Mamilioni Yemen yamkini wakafariki kutokana na mzingiro uliowekwa na Saudia

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula Dunaini, WFP, limeonya kuwa mamilioni ya watu wa Yemen wanakabiliwa na hatari ya mauti kufuatia mzingiro uliowekwa na Saudi Arabia dhidi ya nchi hiyo na hivyo kuzuia misaada kuwafikia wanaohitajia.
Katika taarifa mkuu wa WFP amesema mamilioni ya watu Yemen sasa wanategemea misaada ya kibinadamu ili kuendelea kuishi.
Ameongeza kuwa kati ya watu wote milioni 26 wa Yemen, milioni 17 hawajui mlo wao ujao utatoka wapi huku milioni saba kati yao wakitegemea kikamilifu misaada ya chakula.
Novemba 6 Saudi Arabia ilitangaza kufunga mipaka yote ya anga, nchi kavu na baharini ya Yemen baada ya wapiganaji wa Yemen kuvurumisha kombora hadi katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Riyadh ikiwa ni katika oparesheni ya kulipiza kisasi jinai za Saudia dhidi ya Wayemen.
Watoto ni waathirika wakuu wa jinai za Saudia nchini Yemen
Saudia ilianzisha hujuma yake dhidi ya Yemen mnamo Machi mwaka 2015 kwa uungaji mkono wa Marekani kwa lengo la kuirejesha madarakani serikali kibaraka ya Abdu Rabuh Mansour Hadi aliyejiuzulu urais na kukimbilia mji mkuu wa Saudia, Riyadh. Hivi sasa Saudia inadhibiti mipaka yote ya Yemen na kutumia uwezo huo kuzuia misaada kuwafikia mamilioni ya watu wa nchi hiyo wanaokabiliwa na njaa.
Raia zaidi ya elfu 13  wa Yemen wameuawa, hasa wanawake na watoto, na maelfu ya wengine kujeruhiwa katika uvamizi huo wa kijeshi huku Umoja wa Mataifa ukishindwa kuchukua hatua yoyote ya kuzuia jinai hizo za Saudia huko Yemen. Aidha watu zaidi ya laki sita wameambukizwa ugonjwa wa kipindupindu kote Yemen huku wengine zaidi ya 2,000 wakifarikia dunia tokea mwezi Aprili mwaka huu.

Mamilioni Yemen yamkini wakafariki kutokana na mzingiro uliowekwa na Saudia Mamilioni Yemen yamkini wakafariki kutokana na mzingiro uliowekwa na Saudia Reviewed by RICH VOICE on Novemba 20, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...