Mkufunzi wa Sevilla aliyepatikana na saratani kufanyiwa upasuaji

Mkufunzi wa Sevilla aliyepatikana na saratani kufanyiwa upasuaji

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMkufunzi wa Sevilla aliyepatikana na saratani kufanyiwa upasuaji
Mkufunzi wa Sevilla Eduardo Berizzo atafanyiwa upasuaji siku ya Jumanne baada ya kupatikana na saratani ya tezi dume mapema mwezi huu.
Hali ya mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 48 ilitangazwa baada ya kikosi chake kutoka nyuma na kupata sare ya 3-3 dhidi ya Liverpool katika kombe la vilabu bingwa wiki iliopita.
Sevilla inasema kuwa kurudi kwa Berizzo kutategemea muda atakaochukua kupona upasuaji huo.
Naibu mkufunzi wake Ernesto Marcucci ataiongoza timu hiyo kwa sasa.
Berizzo aliteuliwa kuwa mkufunzi wa Sevilla msimu huu kwa kandarasi ya miaka miwili baada ya kuifunza Celta vigo kwa takriban miaka mitatu.
Mkufunzi wa Sevilla aliyepatikana na saratani kufanyiwa upasuaji Mkufunzi wa Sevilla aliyepatikana na saratani kufanyiwa upasuaji Reviewed by RICH VOICE on Novemba 28, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...