Jeshi la Zimbabwe: Tunawalenga wahalifu sio Mugabe

Jeshi la Zimbabwe: Tunawalenga wahalifu

Image captionJeshi la Zimbabwe: Tunawalenga wahalifu
Jeshi la Zimbabwe limesoma taarifa kwenye kituo cha runinga cha serikali ZBC, likisema kuwa linachukua hatua ya kuwalenga wahalifu.
Hata hivyo limesema kuwa hayo sio mapinduzi ya kijeshi na Rais Mugabe yuko salama.
Milio mikubwa ya risasi ilisikika katika maeneo ya kaskazini mwa mji mkuu Harare mapema leo.
Taarifa hiyo ya jeshi ilikuja saa kadhaa baada ya jeshi kudhibiti kituo cha ZBC.
Mwanamume mmoja ambaye alikuwa amevaa sare za jeshi alisema kuwa jeshi linataka kukabiliana na watu ambao wanatenda uhalifu unaoleta madhara ya kijamii na kiuchumi nchini Zimbabwe.
"Wakati tutakapomalzia wajibu wetu, tunatarajia kuwa hali itadudi kuwa sawa."
Taarifa hiyo ilisema kuwa Mugabe 93, na familia yake wako salama.
Wanajeshi wakiwa na silaha nzito wameoneakana wakirandaranda mjini Harare
Image captionWanajeshi wakiwa na silaha nzito wameoneakana wakirandaranda mjini Harare
Haijulikani ni nani anaongoza hatua hiyo ya kijeshi.
Magari ya wanajeshi waliojihami kwa silaha yameonekana maeneo ya mjini Harare.
Hali hiyo ya wasi wasi wa lolote kuweza kutokea, imeanza hapo jana jioni, ambapo wanajeshi wakiwa na silaha walionekana wakijipanga katika maeneo kadhaa pamoja na kuzingira ofisi za shirika la utangazaji la Zimbabwe ZBC.
Hata hivyo taarifa zinasema kuwa wafanyakazi wa shirika hilo la utangazaji ZBC, waliambiwa na wanajeshi hao kwamba hawapaswi kuwa na wasiwasi na kwamba uwepo wa vikosi hivyo ni kwa lengo la kulinda eneo hilo.
Milipuko mizito imeendelea kusikika pia.
Mkuu wa jeshi la Zimbabwe Constantino Chiwenga alitahadharisha uwezekano wa jeshi kuchukua nchi
Image captionMkuu wa jeshi la Zimbabwe Constantino Chiwenga alitahadharisha uwezekano wa jeshi kuchukua nchi
Chama tawala nchini Zimbabwe kimemtuhumu mkuu wa majeshi Constantino Chiwenga, kwa hatua yake ya madai kuwa jeshi lipo tayari kuingilia mzozo huo wa kisiasa kwa lengo la kulinda wapigania uhuru wa taifa hilo.
Hakuna kauli yoyote iliyotolewa na Rais Robert Mugabe kutokana na hali ya sasa nchini mwake.
Marekani imesema kuwa inafuatilia kwa karibu hali ya Zimbabwe na kutoa rai pande zote kutatua mzozo huo kwa njia ya amani.
Grace Mugabe anaonekana kukaribia kukirithi kiti cha mumewe
Image captionGrace Mugabe anaonekana kukaribia kukirithi kiti cha mumewe
Naye Balozi wa Marekani nchini Zimbabwe kupitia ukurasa wake wa Tiwtter amesema kuwa leo watasitisha shughuli za kiofisi ubalozini hapo kutokana na halisi ya sasa mjini Harare.
Balozi wa Zimbabwe nchini Afrika Kusini Isack Moyo ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa serikali ipo imara katika jambo hilo na kuzuia uwezekano wowote wa kufanyika kwa mapinduzi.
CHANZO:BBC SWAHILI
Jeshi la Zimbabwe: Tunawalenga wahalifu sio Mugabe Jeshi la Zimbabwe: Tunawalenga wahalifu sio Mugabe Reviewed by RICH VOICE on Novemba 15, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...