Mugabe aonekana hadharani kwa mara ya kwanza

Mugabe aonekana hadharani kwa mara ya kwanza



Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMugabe aonekana hadharani kwa mara ya kwanza

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu jeshi la nchi hiyo lichukue madaraka siku ya Jumatano.
Alihudhuria sherehe za kufuzu kwenye mji mkuu Harare.
Bwana Mugabe amekuwa chini ya kuzuizi cha nyumbani kwa siku siku kadhaa huku kukiwa na mvutano kuhusu ni nani atamrithi.
Jeshi lilisema Ijumaa kuwa lilikuwa kwenye mazungumzo na Mugabe na litaujulisha umma kuhusu matokeo ya mazunngumoz hayo haraka iwezekanavyo.
Mtu moja aliyeshuhudia alinukuliwa na Reuters akisema kuwa Mugabe alishangiliwa wakati wa sherehe baada ya kuzungumza.
Jeshi lilichukua madaraka baada ya Mugabe kmfuta kazi makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa wiki iliyopita, na kuashiria kuwa alimpendelea mkewe kuweza kuchukua ungonizi wa Zanu-PF na urais.
Mugabe aonekana hadharani kwa mara ya kwanza Mugabe aonekana hadharani kwa mara ya kwanza Reviewed by RICH VOICE on Novemba 18, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...