Mugabe 'akataa wito wa kumtaka ajiuzulu'

Mugabe (wa pili kulia) akiwa kuzuizi cha nyumbani akisimama na mkuu wa majeshi Constantino Chiwenga (kulia)


Haki miliki ya pichaAFP / ZBC
Image captionMugabe (wa pili kulia) akiwa kuzuizi cha nyumbani akisimama na mkuu wa majeshi Constantino Chiwenga (kulia)

Rais wa miaka mingi nchini Zimbabwe anaripotiwa kukataa kuandoka madarakana mara moja licha ya kuongezeka wito wa kumtaka ajiuzulu.
Mugabe, 93 aliwekwa chini ya kuzuizi cha nyumbani wakati jieshi lilichukua madaraka siku ya Jumatano kufuatia mvutano kuhusu ni nani atamrithi.
Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusu mazungumzo yaliyofanywa Muganbe na ujumbe kutoka kanda hiyo pamoja na mapema.
Lakini taarifa zinasema kuwa amekataa kuondoka madarakani.
Kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai alisema mapema kuwa kwa manufaa ya watu Mugabe anastahili kujiuzulu mara moja.

Robert Mugabe alikutana na mkuu wa majeshi aliyeongoza hatua dhidi yakeHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRobert Mugabe alikutana na mkuu wa majeshi aliyeongoza hatua dhidi yake

Jeshi lilichukua hatua baada ya Rais Mugabe kumfuta makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa, wiki iliyopiya, na kuashiria kuwa alimpendelea mke wake Grace Mugabe, kuchukua uongozi wa chama cha Zanu-PF na kuwa rais.
Taarifa zinasema kuwa Mugabe ambaye alikuwa madarakani tangu nchi hiyo ipate uhuru mwak 1980 anakataa kuondoka kwa hiari kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuandaliwa mwaka ujao.
Baadhi ya wadadisi wanasema kuwa Bw. Mugabe anaweza kujaribu kujihakikishia usalama na familia yake kabla ya kuondoka madarakani.
Maafisa wa Zanu PF mapema walikuwa wamesema kuwa Bw. Mugabe atasalia madarakani hadi ufanyika mkutano mkuu wa Chama mwezi Disemba wakati Bw. Mnangagwa atakiongoza chama na hatimaye kuwa rais

Bw Mugabe alikutana na maafisa katika ikulu ya HarareHaki miliki ya pichaZIMBABWE HERALD
Image captionBw Mugabe alikutana na maafisa katika ikulu ya Harare
Mugabe 'akataa wito wa kumtaka ajiuzulu' Mugabe 'akataa wito wa kumtaka ajiuzulu' Reviewed by RICH VOICE on Novemba 17, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...