Jeshi laonya kuhusu mgogoro ndani ya Zanu-PF Zimbabwe



kamanda mkuu wa jeshi nchini Zimbabwe Jenerali Constantino ChiwengaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionkamanda mkuu wa jeshi nchini Zimbabwe Jenerali Constantino Chiwenga

Kamanda mkuu wa jeshi la Zimbabwe ameonya kuingilia kati iwapo pande pinzani zitaendelea kuzozana ndani ya chama tawala cha Zanu-PF.
Katika taarifa isio ya kawaida , Jenerali Constantino Chiwenga ametaka kusitishwa kwa vita dhidi ya wanachama waliopigania uhuru wa taifa hilo.
Matamshi yake yanajiri baada ya rais Robert Mugabe kumfuta kazi makamu wake wa rais aliyetarajiwa kumrithi Emmerson Mnangagwa.
Kufutwa kwake kunampatia bi Grace Mugabe fursa kumrithi kiongozi huyu mwenye umri wa miaka 93.
Bwana Mnangagwa amelitoroka taifa hilo akihofia maisha yake.
Akizungumza katika makao makuu ya jeshi , jenerali Chiwenga alisema: Mgogoro unaoendelea unaowalenga wanachama wa chama hicho waliopiganai uhuru ni lazima ukome.
''Tunawakumbusha wale wanaofanya hivyo kwamba inapofikia wakati wa kulinda uhuru wetu jeshi halitasita kuingilia kati''.
Jeshi laonya kuhusu mgogoro ndani ya Zanu-PF Zimbabwe Jeshi laonya kuhusu mgogoro ndani ya Zanu-PF Zimbabwe Reviewed by RICH VOICE on Novemba 14, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...