Davido ampiku Wizkid kushinda tuzo ya MTV

Nyota wa muziki nchini Nigeria Davido
Image captionNyota wa muziki nchini Nigeria Davido
Nyota wa Nigeria Davido amempiku Wizkid na kushinda tuzo la muziki za Ulaya MTV na kutuzwa kama mwanamuzik bora wa Afrika.
Davido na Wizkid wameteuliwa kwa tuzo hizo mara mbili wakiwa pamoja.
Davido alikuwa akiwatumbuiza mashabiki wake katika mji mkuu wa Luanda nchini Angola wikendi hii kwa hivyobasi hakuweza kupata fursa ya kushiriki tamasha hiyo.
Lakini amewashukuru kila mmoja ikiwemo mamake kupitia chapisho lake kwenye mtandao wa picha wa Instagram:
Kwenye chapisho lililosema niko FiAAAAAAA!!! Akizungumzia wimbo wake mpya wa FIA:
Washindani wenzake walioteuliwa katika tuzo hizo ni pamoja na Nasty C na Babes Wodumo kutoka Africa Kusini, Nyashinski kutoka Kenya na C4 Pedro wa Angola.
FROM NIGERIA.
Davido ampiku Wizkid kushinda tuzo ya MTV Davido ampiku Wizkid kushinda tuzo ya MTV Reviewed by RICH VOICE on Novemba 13, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...