Muuguzi alipwa dola 500,000 katika kisa cha kukataa mgonjwa kutolewa damu

Nurse Alex Wubbels is shown during an incident at University of Utah Hospital in Salt Lake City, Utah, U.S., in this still photo taken from police body-worn camera video taken July 26, 2017

Haki miliki ya pichaPRESS EYE
Muuguzi mmoja ambaye alikamatwa baada ya kukataa kumruhusu polisi kuchukua sampuli ya damu kutoka kwa mgonjwa ambaye alikuwa amepoteza fahamu amekubali fidia ya dola 500,000.
Alex Wubbels aliafikia makubaliano hayo ya fidia na mji wa Salt Lake na chuu kikuu cha Utah, kwa mujibu wa wakili wake.
Kukamata kwake na polisi mwezi Julai kulizua ghadhabu baada ya video ya kisahicho kuibuka baadaye. Ananaka akiwa na pingu mikononi huku akisukumwa na polisi kwenda kwa gari.
Baadaye aliachiliwa bila ya kushtakiwa. Polisi aliyemkamata alifutwa kazi mwezi uliopita huku mkubwa wake akishushwa madaraka.
Polisi Jeff Payne alitumwa kwenda hospitali ya chuo cha Utah tarehe 26 mwezi Julai kuchukua sampuli ya damu kutoka kwa dereva ambaye alikuwa amehusika kwenye ajali ya barabarani na ambaye alikuwa amepoteza fahamu.
Jeff Payne (L) and James TracyHaki miliki ya pichaSALT LAKE CITY POLICE
Image captionDetective Jeff Payne (L) was fired and James Tracy, his watch commander, was demoted two ranks
Mgonjwa hakuwa ameshukiwa kufanya lolote baya.
Bi Wabbels ambaye alikuwa zamu wakati huo alimuambia polisi Payne kuwa hakuwa na waranti wa kuchukua sampuli ya damu jinsi inavyohitajika na sera za hospitali na sheria za jimbo.
Pia alisema kuwa damu haingechukuliwa bila ya idhini ya mgonjwa.
Bi Wubbels alikataa kumuambia polisi alikokuwa mgonjw au kumruhusu kuchukua damu.
Luteni James Tracy kisha akamuamrisha Det Payne kumkamata Bi Wubbels.
Hospitali ya chuo cha Utah baadaye ilisema kwa ilikuwa imeleta sera mpya zinazowazuia polisi kuingia hospitalini wenyeee kuchukua sampuli ya damu.
Muuguzi alipwa dola 500,000 katika kisa cha kukataa mgonjwa kutolewa damu Muuguzi alipwa dola 500,000 katika kisa cha kukataa mgonjwa kutolewa damu Reviewed by RICH VOICE on Novemba 01, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...